Header Ads

Arsene Wenger na Maurcio Pochetino katika vita kubwa ya maneno


Kocha wa Arsenal wiki hii alitoa kauli ambayo imepokelewa vibaya na mashabiki wa Tottenham, wiki hii nzima mashabiki wa Tottenham mitandaoni wamekuwa wakimuandama Wenger.
Wakati Wenger akiongea na waandishi wa habari alisema anashangazwa na jinsi waandishi wanavyoongea kuhusu Arsenal kukosa makombe na huku kuna vilabu kama Tottenham na Liverpool nao wako hivyo hivyo.
Kocha wa Tottenham ameisikia kauli ya Wenger na kusema kwamba badala ya Wenger kujihusisha na kufuatilia mambo ya Tottenham inambidi awaze yeye kwanza kuhusu uwezo wao uwanjani.
Pochettino amesisitiza kwamba anamuheshimu sana Arsene Wenger na asingependa kupoteza heshima yake kwa kumuongelea vibaya lakini kwa sasa anaona ni vyema azungumzie masuala ya Arsenal zaidi.
Tottenham hawajachukua CL tangu mwaka 1984, hawajachukua EPL 1960/1961 na hawajachukua kombe la ligi tangu msimu wa 2007/2008 lakini Pochettino amesisitiza kwamba timu sio makombe tu ila hata wanavyokua ni jambo zuri.

No comments