Header Ads

Tetesi za usajili barani Ulaya



Baada ya Alexis Sanchez kuondoka Arsenal sasa klabu hiyo iko tayari kutuma ofa kwa PSG kwa ajili ya kumnunua Lucas Moura ambaye Arsene Wenger anamuona kama mtu sahihi wa kuvaa viatu vya Sanchez.
Inadaiwa kwamba mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Olivier Giroud anaweza kufanya usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Aubameyang usitokee kwani hana mpango wa kwenda Dortmund.
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amekiri kwamba kwa sasa kazi yake haiko mashakani sana lakini amekiri kwamba mechi yao na PSG inaweza kuamua hatma yake ndani ya klabu hiyo ya Real Madrid.
Real Madrid wanataka kurudi tena kwa Manchester United kumuwinda mlinda lango wao David De Gea na taarifa zinasema kwamba tayari Madrid wameshamwambia wakala wa De Gea kuhusu nia yao hiyo.
Pep Gurdiola anatajwa kuingia kwenye vita ya kumnasa Antoine Griezman toka Atletico Madrid na Manchester City wanataka kumtumia Kun Aguero aende Atletico na wao wamchukue Mfaransa huyo.
Klabu ya As Roma imekanusha taarifa kwamba wamekubaliana ada ya uhamisho na Chelsea, wakati huo huo wakala wa Dzeko anadaiwa kushindwa kusafiri kwenda Uingereza kutokana na matatizo ya Visa na hivyo Chelsea itawabidi kusubiri hadi ashughulikie tatizo hilo.
Jose Mourinho anaonekana anataka tena kuingilia uhamisho wa Chelsea na sasa amepanga kuwapa upinzani kumnunua mlinzi wa kushoto wa Juventus Alex Sandro anayetajwa kuwa mrithi wa Luke Shaw.

No comments