Header Ads

Buswita na wenzake 6 kuikosa Azam



Taarifa rasmi ya kutoka klabu ya Yanga inaeleza kuwa, wachezaji saba (7) wa klabu hiyo wataukosa mchezo wa ligi kuu Tamzania bara dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex.
Afisa habari wa Yanga Dismas Ten ametaja sababu mbalimbali zinazowafanya wachezaji hao waukose mchezo huo ikiwa ni pamoja na majeruhi, kuumwa pamoja na kadi.
“Thabani Kamusoko, Yohana Mkomola, Amis Tambwe, Donald Ngoma, Pato Ngonyani na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ wanakabiliwa na majeraha wengine wanaumwa lakini Pius Buswita yeye ana kadi tatu za njano”-Dismas Ten, afisa habari Yanga.
Ten amesema uongozi umefanyia kazi suala la kibali cha kufanyia kazi cha kocha wao mkuu ambaye hajakaa kwenye benchi katika mechi mbili zilizopita tangu amerejea nchini akitokea kwao Zambia kwa ajili ya mazishi ya mtoto wake.
“Kuhusu suala la kibali cha mwalimu tayari kimefanyiwa kazi na taratibu zoye zimefuatwa hivyo mashabiki na wanachama waondoe shaka juu ya jambo hilo.”

No comments