Zidane hashikiki Madrid, hiki ndicho alichowafaanyia katika mechi zake 100
Ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Getafe ilikuwa ndio mechi ya 100 kwa Mfaransa Zinedine Zidane tangu apewe kijiti cha ukocha katika klabu hiyo akipokea mikoba ya kocha aliyetangulia Raphael Benitez.
Katika michezo yake 100 ambayo Zidane ameifundisha Los Blancos ameshinda michezo 75 huku akitoka sare michezo 17 na michezo 8 tu kati ya hiyo 100 ndiyo michezo aliyopoteza Zinedine Zidane.
Mwaka 2016 alibeba Champions League akalitetea 2017, msimu wa mwaka 2016/2017 akawapa Madrid kombe la ligi kuu nchini Hispania La Liga huku pia 2016/2017 akawapa tena Super Cup.
2016 aliwapa Real Madrid kombe la klabu bingwa dunia na 2017 tena akawapa kombe la Super Copa la nchini Italia na kumfanya kuwa kati ya makocha bora kuwahi kukaa katika benchi la Real Madrid.
Lakini Zinedine Zidane pia ameweka rekodi ya kutofunga mechi 40 akiwa na Real Madrid mwaka 2016 April hadi January 2017 na mwezi wa pili mwaka jana akaweka rekodi ya kushinda michezo 13 ya ugenini mfululizo.
Zidane pia kati ya michezo hiyo 100 kuna michezo 73 ambayo Real Madrid walifunga goli kila mchezo rekodi ambayo ilidumu kuanzia April mwaka 2016 hadi mwezi uliopita walipocheza na Real Betis.
Katika michezo yote ambayo Zinedine Zidane ameifundisha Real Madrid mfungaji bora amekuwa Cristiano Ronaldo mbaye katika kipindi hicho amecheza michezo 78 na kufunga mabao 74, Benzema akifuatia na magoli 32.
Japokuwa makocha waliomtangulia Zidane kama Carlo Ancelotti na Jose Mourinho walishinda michezo mingi lakini walipoteza pia mechi nyingi kuliko Zidane.
Carlo Ancelotti katika mechi zake 100 za mwanzo Real Madrid alipata ushindi mara 78 akapata suluhu mara 10 huku akifungwa mara 12, Mourunho akishinda mara 77, suluhu 13 na vipigo mara 10.
Msimu huu Zidane amepigwa mara moja akapata suluhu mara mbili akishinda michezo 5 na kumfanya kushika nafasi ya pili akiwa na alama 5 nyuma ya vinara Barcelona.
Post a Comment