KISA UMATI WA WATU, LULU AMPIGIA SALUTI ZARI!
Ule msemo wa nabii hakubaliki kwao! Umeweza kujidhihirisha kwa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ambaye juzi alituaBongo akitokea South Afrika nakupokelewa kwa nderemo na vifijo na umati mkubwa wa watu, ambapo umati huo ukajitokeza tena jana katika ukumbi wa Mlimani City, alipotinga kwa ajili ya kuzindua kampuni ya DANUBE, hali hiyo ya kupokelewa mithili ya Mfalme, imemshtua Divakutoka kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Ambaye amempigia saluti Zari na kusema mastaa wa Bongo hawana budi kumpenda tu, kwani licha ya kuwa siyo Mbongo ila ana mashabiki wengi Bongo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lulualipost picha ya Zari na kuambatanisha na maneno yanayoashiria kushangazwa na jinsi mwanamama huyo alivyopokelewa na Watanzaniakama vile ni Mtanzania halisi.
Kama ilivyo kawaida ya mashabikibaada ya kuiona Post hiyo hawakumuacha salama Lulu, wakamporomoshea koment za kumchamba kuwa anajipendekeza kwa mtu ambaye hana shobo na mastaa wa Bongo.
Post a Comment