Header Ads

Video 5 za Bongo Flava ‘zinazotrend’, Diamond bado king’ang’anizi


Mambo vipi? kama kawaida ni juma nne nyingine tena nakuletea chart ya video tano kali za Bongo Flava ‘zinazotrend’ katika mtandao wa YouTube, let’s go!!
Katika Chat ya wiki hii hakuna mabadiliko makubwa zaidi ya ngoma mpya ya Mwana FA, AY & Fid Q – Upo Hapo? ambayo imeingia kwa mara ya kwanza, ila stori ni kwamba ngoma ya Diamond ft Morgan Heritage – Hallelujah imeonekana kuwa king’ang’anizi baada ya kukaa kwenye chati kwa wiki tatu sasa.
  1. Harmonize ft Korede Bello –  Shulala (katika trending ya Tanzania pia ni namba 1 na wiki iliyopita ilikuwa katika nafasi hiyo.

2. Mwana FA, AY & Fid Q – Upo Hapo? (katika trending ya Tanzania ni namba 3),  wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na  Aslay – Natamba.

3.  Aslay – Natamba (katika trending ya Tanzania ni namba 8), wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Diamond Platnumz ft Morgan Heritage – Hallelujah.

4. Diamond Platnumz ft Morgan Heritage – Hallelujah (katika trending ya Tanzania ni namba 39), wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Madee ft Nandy – Sema.

5.  Madee ft Nandy – Sema (Wiki iliyopita nafasi hii ilishikiliwa na Kala Jeremiah ft Kalumbu – Vijana.

No comments