Header Ads

Matokeo ya michezo yote ya EPL wikiendi hii


Hapo jana siku ya Jumapili michezo kadhaa imepigwa katika ligi kuu nchini Uingereza ambapo klabu ya Arsenal imechomoza na ushindi wa mabao 5-2 dhidi  Everton ikiwa ugenini katika dimba la Goodison Park huku wenyeji wakiongozwa na Wayne Rooney wakishindwa kuokoa jahazi la timu hiyo lililokuwa likizama EPL.
Everton dhidi ya Arsenal 5-2
Katika matokeo ya michezo mingine Tottenham imechomoza na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Liverpool katika dimba la Wembley.
Tottenham dhidi ya Liverpool 4-1 
Michezo iliyopigwa siku ya Jumamosi ni
Na huko Stamford Bridge mabingwa watetezi wa ligi kuu ya nchini Uingereza klabu ya Chelsea imechomoza na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Watford.
Chelsea dhidi ya Watford 4-2
Wakati kikosi cha mreno, Jose Mourinho klabu ya Manchester United hapo juzi siku ya Jumamosi imewashangaza wengi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Huddersfield wakiwa ugenini na kuwa ndiyo mchezo wake wa kwanza kupoteza katika ligi ya Uingereza msimu huu.
Manchester United ikifungwa 2-1 dhidi ya Huddersfield
Klabu ya Manchester City imechomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley.
Manchester City ikiifunga Burnley mabao 3-0
Huko Newcastle klabu hiyo imeifunga timu ya Crystal Palace bao 1-0 lilifungwa na mchezaji, Mikel Merino.Stoke ikiwa nyumba imekubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth magoli ya kifungwa na Andrew Surman na Junior Stanislas.
Newcastle imechomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace
Wakati katika dimba la Liberty kikosi cha Leicester kimeifunga timu ya Swansea kwa jumla ya mabao 2-1 huku meneja wa timu hiyo, Michael Appleton akichomoza na ushindi wake wa kwanza toka aanze kukiongoza kikosi hicho.
Leicester City  ikiifunga Swansea kwa jumla ya mabao 2-1 
Timu ya Southampton ikiwa nyumbani imechomoza na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya West Brom bao la dakika za mwisho la Sofiane Boufal likaipa ushindi.
Southampton ikiwa nyumbani imechomoza na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya West Brom

No comments