Header Ads

Unayopaswa kujua kueleka The Best Fifa 2017 usiku wa leo, nani kuchukua na nani kukosa?


Usiku wa leo katika jiji la London kunaenda kufanyika tukio kubwa sana katika soka, shirikisho la soka duniani linakwenda kutoa tuzo kwa makocha na wachezaji waliofanya vizuri mwaka 2017.
Pamoja na kuwepo kwa tuzo nyingi lakini macho ya wengi yatakuwa katika kinyann’anyiro cha The Best Fifa Male awards ambapo Lioneil Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar Dos Santos wanawania tuzo hiyo.
Kwa mafanikio waliyopata katika msimu uliopita wa ligi Cristiano Ronaldo anapewa nafasi kubwa kubeba tuzo hii kutokana na msaada aliowapa Real Madrid katika Champions League pamoja na michuano ya La Liga.
Tuzo hizi za Fifa zimekuja baada ya Fifa kuacha ushirikiano wao na jarida la Ballon D’Or na Ronaldo De Lima na Zinedine Zidane ndio wamechukua tuzo hii mara nyingi (3) na kama Cr7 atachukua tuzo hii atakuwa amewafikia.
Mshindi katika tuzo hizi anapatikana kwa kupigiwa kura ambapo kura zinapigwa na mashabiki, makocha,waandishi wa habari za michezo na macaptain ambapo kila kundi limepewa 25%.
Katika tuzo hizi kuna mwanadada raia wa Venezuela Deyna Castellanos mwenye miaka 18 ambaye yeye sio mwanasoka katika klabu kubwa lakini goli alilofunga akikitumikia chuo chake cha Florida lilimfanya dunia imtambue na kupewa nafasi.
Deyna anasema hakuwahi kuwaza kuweponkwenye tuzo hizo na hata siku majina yanatangazwa alikosa nguvu aliposikia jina lake likiwepo katika majina ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kike.
Deyna Castellanos yupo katika kinyang’anyiro chake akigombea tuzo hiyo pamoja na Lieke Martens na Carli Lloyd ambaye anapewa nafasi kubwa kunyakua tuzo hiyo.
Deyna Castellanos pia bao alilofunga chuoni kwao limeingia kwenye kinyang’anyiro cha bao bora huku akikumbana na upinzani kutoka kwa Olivier Guroud bao lake la nge na Ocarine Masuruke bao dhidi ya Orlando Pirates.
Antonio Conte kombe la kwanza katika msimu wake wa kwanza Epl  linamuweka katika kinyang’anyiro cha kocha bora akipambana na Massimiliano Allegri na Zinedine Zidane.
Idris Elba muigizaji wa filamu kubwa kama vile The Jungle Booka na Thor atakuwa ndio host wa tuzo hizi kubwa katika soka, nani atachukua na na nani atakosa? Tuonane baadae.

No comments