Header Ads

Nachukia umalaya – Gigy Money



Msanii wa Bongo Fleva na Video Queen, Gigy Money amefunguka kuwa moja ya vitu anavyovichukia katika maisha yake ni umalaya huku akidai tabia hiyo inashusha hadhi ya mwanamke.
Gigy Money na Amber Lulu jana kwenye party ya mtoto wa Hamisa Mobetto.
Gigy Money amesema anajua kuwa kuna wanawake wanaishi mjini kwa kazi hiyo lakini yeye hawezi kufanya kazi hiyo na ndio kazi anayoichukia maishani mwake.
Nachukia sana kazi ya umalaya najua watu wengi hasa wasichana wengi wanaifanya na wanaipenda ila haina faida kubwa, faida yake ni ya muda mfupi,“amesema Gigy Money kwenye mahojiano yake na hamisihemedi.com jana (Ijumaa) kwenye sherehe ya Mtoto wa Hamisa Mobetto.
Hata hivyo, Gigy Money amekiri wazi kuwa alishawahi kudanga kipindi cha nyuma lakini kwa sasa ameacha tabia hiyo.

No comments