NUH MZIWANDA AANDIKA WARAKA MZITO KWA MTOTO WAKE!
Siku zote Tembo wakipigana zinazoumia nyasi! Hicho ndicho kinachoendelea kati ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, na aliyekuwa mkewe Nawal, ambapo baada ya kutengana kwao, Nuh anadai kuwa mtoto wao Anyaghile anateseka na ameonyesha hisia za kuumizwa na kutokuwa karibu na mwanae, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe ufuatao.
Dhumuni la waraka aliouandika Nuhkwa mwanae, ni kumtaka atakapokuwa hapo baadaye ajue kuwa hakumtelekeza ili hata mama yake atakapojaribu kumjengea chukikuwepo na ushahidi wa kuthibitisha kuwa siyo kweli.
Baada ya post hiyo, baadhi yamashabiki walionyesha kuguswa na ujumbe wake na wakakoment kwa kumpa pole, huku wengine wakimbeza kwa kumwambia huenda amemmis mzazi mwenziye na si mtoto kama anavyosema.
Post a Comment