MOTO WA FIESTA KUWAKA SONGEA LEO
BAADA ya moto mkali kuwashwa jijini Mbeya, hatimaye wakazi wa Songea watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanauzima moto leo katika Uwanja wa Majimaji ambapo wasanii kama Jux, Ben Pol, Nandy, Maua, Vee Money, Mimi Mars na wengineo watauwasha.
Mmoja wa waratibu wa Fiesta 2017, Fauzia Abdi amejinadi kuwa, wakazi wa Songea wajipange kikamilifu katika suala la burudani kwani wasanii takribani wote waliofanya makamuzi jijini Mbeya wa t a u n gana na wengine w a p y a kuuwas h a moto k a t i k a uwanja huo wa Majimaji baada ya kukosekana burudani hiyo kwa misimu miwili mfululizo.
“Kutakuwa na ‘surprise’ kibao hiyo siku maana kuna wasanii hatujawataja hapa lakini wasishangae kukutana na mtu ambaye wao hawakumtarajia maana kazi yetu siku zote imekuwa ni kufanya kila liwezekanalo ili tuwaburudishe vya kutosha,” alisema Fauzia.
Wasanii wengine ni G-Nako, Stamina, Roma, Darasa, Aslay, Dogo Janja, Ommy Dimpoz ,Bright na Nchama ambao watapafomu.
Post a Comment