JUUKO NA MAVUGO SI MCHEZO, NI KAZIKAZI KAMA MECHI
Ingawa hajasema popote lakini Kocha Joseph Omog anaonekana amepania kuhakikisha mshambuliaji wake, Laudit Mavugo anakuwa katika kiwango bora.
Mavugo ni kati ya washambuliaji wazuri kutokana na vitu alivyonavyo kama kasi, mashuti, ukaaji wa kwenye nafasi na kadhalika lakini hajawa na matokeo mazuri sana.
Kutokana na hali hiyo, Kocha Omog amekuwa akihakikisha anampanga timu tofauti na beki Juuko Murshid.
Mrundi huyo amekuwa na kazi ngumu ya kumpita Juuko mazoezini kwa kuwa beki huyo ni imara na matata.
Kutokana na ushindani huo, kawaida unamfanya Mavugo kuwa imara zaidi na itamsaidia kufanya vizuri katika mechi.
Ukiona Mavugo na Juuko wanachuana mazoezini inakuwa utafikiri ni mechi.
Post a Comment