Header Ads

Rb Leizpg waisadia Bayern Munich kufika kileleni


Mchezo wa kwanza wa kocha Jupp Heynckess tangu arudi Bayern Munich kwa mara nyingine kuchukua mikoba ya Carlo Ancelotti aliyetimuliwa inashuhudiwa Bayern wakiipa Freiburg bao 5.
Inaonekana kama bahati au kuilewa zaidi Bayern kwani kocha huyu mkonge kwa siku ya kwanza tu anawafanyabwaonekane uwanjani kama Bayern ile iliyochukua makombe matatu chini yake 2013.
Baada ya mchezo huo Jupp anaongea na waandishi wa habari na kusisitiza kwamba ana kikosi bora sana kuliko kile ambacho alichukua nacho makombe mwaka 2013.
Bao la kujifunga la Schutter na mengine ya Kimmich, Lewandoski, Thiago Alcantara na Coman yalionesha Bayern wanavyoshambulia kupitia kwa kila mtu hali iliyochangia kuwaadhiri Freiburg.
Lakini pia hakuna marefu yasiyo na ncha na ndivyo hivyo kwa Borussia Fortmund kwani baada ya kutopigika katika michezo 7 iliyopita hatimaye RB Leizpg walimaliza ufalme wao na kukata rekodi yao.
Mchezo wa kuvutia sana huku Pierre Aubemayang akiongeza idadi ya mabao kwa kufunga mabao mawili ya Dortmund na Leizpg wakifunga matatu kupitia Sabtizer,Poulsen na Augustin.
Mchezo huu ulimalizika kwa wachezaji kubaki 10 kwa kila pande baada ya kuoneshwa kadi nyekundu na sasa Bayern Munich wanakuwa wamebakisha alama mbili kuwakuta Borrusia Dortmund walioko kileleni.

No comments