Header Ads

Kigezo cha umri kimekwamisha usajili wa Mkomola Tunisia


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes, Yohana Mkomola amesema, ameshindwa kujiunga na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa kigezo cha kutofikisha umri wa miaka 18.
Ni kweli nilienda kwenye majaribio nchini Tunisia namshukuru Mungu mambo yalienda vizuri kwenye majaribio hayo kama mara ya kwanza kwa sababu hii ni mara ya pili.
Yalikuwa ni majaribio ya wiku tatu, nashukuru nimefanya vizuri mimi pamoja na wenzangu lakini kucheza ligi ya kwao ni hadi ufukishe miaka 18 ambayo mimi bado sijafikisha. Kwa hiyo hadi nifikishe umri huo ndio nitasaini mkataba na kuanza kucheza ligi yao.
Kwa upande wa wenzangu nafasi yao ilikuwa finyu kutokana na nafasi wanazocheza, walikuwa wanataka washambuliaji lakini wenzangu ni viungo na beki wa kati.
Mkomola atatimiza miaka 18 April 2018 lakini mawasiliano bado yanaendelea vizuri na kila kitu kitakapokuwa sawa huenda akajiunga na klabu hiyo.
August 17, 2017 Mkomola pamoja na Henriq Vitalis na Ally Ng’anzi walisafiri kwenda Tunisia kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye klabu hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa mkomola kupata mwaliko huo lakini ni mara ya kwanza kwa wenzake.

No comments