Amber Lulu adai Prezoo hakuambulia kitu kwake
Video Vixen na msanii wa muziki wa Bongo Flava, Amber Lulu amesema si kweli alitoka kimapenzi na rapper Prezoo kutoka nchini Kenya ambaye alikuwa hapa nchini siku za hivi karibuni.
“Watu wengine washamba lakini ni vitu fulani vya kinyamwezi tu ambapo unaweza ukakaa na mtu chumba kimoja na msifanye kitu chochote,” amesema Amber Lulu.
Aliongeza kuwa ndege wawili wanaofanana huwa wanaruka pamoja kwa hiyo Prezoo ni kama rafiki kwake na hakuna tatizo la wao kuwa hivyo. Aliendelea kwa kusema nyumba walikuwa pamoja ni kama apartment ambapo kila mmoja alikuwa na chumba chake.
Post a Comment