Header Ads

Kichuya kaweka rekodi ya kufunga October 1 mfululizo


Kiungo mshambukiaji wa Simba Shiza Kichuya anejitengenezea rekodi ya aina yake baada ya kufanikiwa kufunga siku ya October 1, katika misimu miwili tofauti.
Leo Jumapili October 1, 2017 Kichuya amefunga goli moja katika ushindi wa Stand United 1-2 Simba katika uwanja wa CCM Kirumba, Shinyanga.
Kama unakumbuka, October 1, 2016 Kichuya alifunga bao la kusawazisha dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika wakati Simba ilipolazimisha sare ya 1-1 na Yanga.
Mchezo wa October 1, 2016 uliambatana na matukio kadhaa ikiwemo la vurugu za mashabiki baada ya goli la Tambwe ambalo lilidaiwa ni la mkono. Vikang’olewa mabomu yakapigwa, Jonas Mkude akatolewa kwa kadi nyekundu iliyokuwa ya utata na baadae ilifutwa.
Mechi ya October 1, 2017 pia umeambatana na maswali mengi, goli lililokataliwa la Laudit Mavugo kwamba lilikuwa ni offside au onside? Lakini pia suala la jezi za Simba na Stand United limezua mijadala sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii kwamba kulikuwa na mfanano wa jezi za timu hizo.

No comments