BREAKING: Tundu Lissu atolewa ICU, anahamishwa nchi
Zifuatazo ni updates kuhusiana na hali ya kiafya ya Mbunge wa Singida Mashariki ambae pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu ambae alipigwa risasi nyumbani kwake Dodoma.
Baada ya kulazwa Hospitali Nairobi Kenya kwa muda wote huo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kimezungumza leo na kusema hali imebadilika.
“Hatukupenda kutoa kila siku taarifa za Mgonjwa ila tuliamini kwamba utakapofika wakati muafaka tutatoa taarifa ya Mgonjwa kwa kiwango ambacho taaluma ile inaturuhusu tutoe” – Mbowe
- Afya ya ndugu yetu Lissu imeendelea kuimarika, alihitaji upasuaji mwingi sana kwenye mwili wake… ni miujiza na imeendelea kuwa miujiza, amefanyiwa upasuaji aina kadhaa mara 17 mpaka dakika hii na kupewa damu nyingi kuliko Mgonjwa yeyote alieingia Hospitali ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita.
- Amekua kwenye chumba cha Wagonjwa Mahututi kwa kipindi chote alichokua Nairobi ambapo wiki iliyopita kwa mara ya kwanza ametoka kwenye chumba hicho cha ICU.
- Mashine zote zilizokua kwenye mwili wake kumsaidia zimeondolewa kwasababu sasa mwili wake una uwezo wa kujisukuma wenyewe, viungo vyake vyote ni timamu.
- Mh. Lissu hatumii tena oxygen kwasababu ana uwezo wa kupumua peke yake, hatumii tena mirija kula chakula na sasa anakula chakula chake anachokitaka yeye mwenyewe.
- Hizo ni baadhi ya kauli kuhusu Lissu ambae juzi kwa mara ya kwanza amefanya kitu ambacho hakuwahi kukifanya toka apigwe risasi, pia kuhusu kuondolewa Kenya na kupelekwa nchi nyingine… bonyeza play hapa chini kupata kila kitu
Post a Comment