Header Ads

Petr Cech ashindwa kuisaidia Gunners katika matuta tangu ajiunge nao


Huwezi kutaja magolikipa watatu wakubwa katika ligi kuu ya Epl ukamuacha mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech ambaye tangu amefika Epl amekuwa na mafanikio makubwa akiidakia Chelsea na hatimaye Arsenal.
Lakini Cech pamoja na uhodari wake langoni ila tangu amejiunga na Gunners anaonekana kupwaya sana huku akiwa mlinda lango mwenye rekodi mbovu zaidi katika ligi kuu katika mikwaju ya penati.
Rekodi zinaonesha tangu Cech asaini Arsenal hajawahi kupangua wala kudaka mkwaju wa penati hata mmoja na penati zote 11 zilizopigwa langoni mwake tangu ajiunge na Arsenal zimekwenda nyavuni.
Hali hii ni tofauti na alipokuwa Chelsea ambapo alifanikiwa kuokoa mikwaju minne ya penati katika ligi ya Epl na huku akicheza mikwaju mitatu katika michuano mikubwa ya Champions League.
Wakati magolikipa wemgine kama David De Gea akiokoa penati mbili kati ya 17 zilizoelekezwa langoni mwake, golikipa wa Liverpool Simon Mignolet ni kinara wa kuokoa penati ambapo hadi sasa ameshacheza penati 7 kati ya 15.
Mwishoni mwa wiki Arsenal walijikuta wakipigwa bao mbili kwa moja na Watford huku bao la kwanza la Watford likiendeleza rekodi mbovu ya Petr Cech kuokoa matuta baada ya Trooy Deney kufunga kwa mkwaju wa penati.

No comments