Header Ads

NGOMA AIPA SIMBA MECHI 5 ZA UBINGWA


Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe.
STRAIKA wa Yanga, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe, amesema kuwa, anatoa mechi tano tu za mwanzo za Ligi Kuu Bara, baada ya hapo ndiyo itafahamika mbio za ubingwa wa msimu huu zimekaaje.
Ngoma ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya msimu huu kuanza huku timu zikiwa zimeshacheza mechi mojamoja ambapo Simba inaongoza msimamo ikiwa na pointi tatu na mabao saba. Kutokana na Simba kuwa kileleni, tayari mashabiki wa timu hiyo wameshaanza kuona mwanga wa kikosi chao kuwa bingwa msimu huu, jambo ambalo Ngoma anasema ni mapema mno kutabiri hivyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ngoma alisema katika ligi hii ambayo kila timu inacheza mechi 30 kumaliza msimu, huwezi kutabiri bingwa ikiwa imechezwa mechi moja tu, bali kwa upande wake anasubiri kuona mpaka zipite mechi tano ndiyo ataona timu ipi inaweza kuwa bingwa. “Kwa sasa timu yetu haipo vizuri kutokana na majeruhi wengi tulionao kama Tambwe (Amissi), Chirwa (Obrey), Beno (Kakolanya) na Mwashiuya (Geofrey), kama hao watakuja kupona wote, nadhani tutakuwa tumekamilika hasa.
“Zamani tulikuwa na tatizo la kiungo mkabaji, lakini tayari limeshatafutiwa ufumbuzi kwa Ngoma aipa Simba mechi 5 za ubingwa Musa Mateja na Omary Mdose kusajiliwa Papy Tshishimbi, hivyo wale waliokuwa majeruhi kama wakipona tutakuwa hatushikiki,” alisema Ngoma. Aidha, Ngoma amekisifia kikosi cha Simba kutokana na usajili uliofanyika huku akimtaja Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi kuwa watakuwa msaada mkubwa kikosini hapo.

No comments