Msanii wa Tanzania, Lady Jaydee
MSANII wa Tanzania, Lady Jaydee, amefunguka mengi juu ya ujio wake mpya wa kurap (kuchana) amesema si kama kaacha ila kaamua kuwabadilishia ladha mashabiki zake hili wasimchoke ndiyo maana kaamua kuja na ujio mpya wa kurap (kuchana).

Na alipoulizwa juu ya ujio wake mpya wa kurap alimefunguka kwamba: “Nimeamua kuchana kwa sababu ya kuwabadilishia ladha mashabiki zangu wasinichoke mapema au wasizoee aina moja ya kuimba.
“Nataka wanijue mimi ni kinyonga kuwa nabadilika kila muda kwa hiyo wasinichoke nikija kwa aina ya uimbaji mwingine,” alisema Lady Jaydee
Aliendelea kufunguka juu ya mtu aliyetengeneza ngoma hii na aliyemshauri kufanya aina hii ya wimbo akisema:
“Napenda kufanya kazi na Man Walter kwa sababu anajua na yeye ndo katengeza huu wimbo, ila kuna baadhi ya maneno kwenye huu wimbo kaniandikia FID Q, Domo Kaya, Credible na mimi mwenyewe.

Kwa hiyo najiamini kufanya wimbo wa kurap na wimbo wangu huu mpya wa kurap unaitwa (I Miss You),” alisema Lady Jaydee
Ni wasanii wachache wa kike wanaochana wanafanya vizuri na wengine hawafanyi vizuri, kikubwa ni kuimba vizuri na mashairi mazuri; basi kila mtu ataupenda huo wimbo kwani watu wanapenda nyimbo nzuri.