Header Ads

Arsenal kwa mara ya kwanza imecheza Europa League baada ya zaidi ya miaka 20

Usiku wa September 14 2017 michezo wa UEFA Europa League hatua ya Makundi msimu wa 2017/2018 ilichezwa barani Ulaya kwa michezo zaidi ya nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali, zaidi ya
miaka 20 usiku wa September 14 2017 tumeishuhudia club ya Arsenal ikicheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Europa baada ya miaka 20.


Arsenal ambao walikuwa katika dimba lao la nyumbani la Emirates dhidi ya Koln FC ya Ujerumani walifanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 3-1, licha ya kuwa wamekuwa hawafanyi vizuri katika michezo yao ya Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 na kuambulia kushinda mechi 2 kati ya mechi 4 walizocheza hadi sasa na wapo nafasi ya 11.

Licha ya kuwa mchezo ulichelewa kuanza kwa sababu ya mashabiki kuleta fujo kidogo, Koln ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 9 kupitia kwa Jhon Cordoba na magoli ya Arsena yalifungwa na Sead Kolasinac dakika ya 49, Alex Sanchez dakika ya 67 na Hector Bellerin dakika ya 82.




Matokeo ya game za Europa League msimu wa 2017/2018 zilizochezwa Alhamisi September 14 2017

No comments