Header Ads

Harry Kane aongoza kwa Hat Trick barani Ulaya


Mabao 23 kati ya 109 ambayo ni sawa na wastani wa 23% ambayo Cristiano Ronaldo amefunga katika Champions League amezifunga timu za Uherumani, hiyo inakuja baada ya usiku huu kuweka kambani bao 2 wakati wakiiua Dortmund bao 3 kwa 1.
Harry Kane naye amezidi kudhihirisha unyama alionao baada ya kuweka hat trick wakati Tottenham wakiifunga Apoel bao 3 kwa 0 na kuwa mchezaji mwenye hat trick nyingi zaidi Ulaya katika msimu huu anazo hat trick 7.
Sevilla wametwa uongozi wa Group E baada ya kupata alama 3 muhimu pale walipoifunga Maribor bao 3 kwa 0 huku Liverpool wakienda sare ya bao moja kwa moja na Spartak Moscow.
Mabao ya Kelvin De Bruyne na Raheem Sterling yaliwapa Man City jumla ya mabao 26 katika michezo yao 7 iliyopita huku usiku huu walipata ushindi wa bao 2 kwa nunge dhidi ya Shaktar Donestki huku Napoli wakiipiga Feyenoord jumla ya mabo 3 kwa 1.

No comments