Sakata la Diego Costa na Chelsea lachukua sura mpya, haya hapa maamuzi ya Chelsea
Msuguano kati ya Chelsea na Diego Costa umechukua sura mpya baada ya klabu hiyo kuamua kumkata mshambuliaji huyo mshahara kwa kosa la kutotokea mazoezini wakati wa pre season.
Taarifa zinasema Diego Costa alipaswa kuwepo katika mazoezi ya timu hiyo wakati wa pre season lakini mwanasoka huyo aligoma kutokea baada ya kutokuelewana na kocha Antonio Conte.
Chelsea wamemkata Costa kiasi cha £300,000 kwa kitendo hicho ikiwa ni siku moja baada ya mshambuliaji huyo kueleza katika mahojiano na jarida moja la Uingereza jinsi alivyokuwa na wakati mgumu chini ya Conte.
Hapo jana Costa alisema alipokuwa Chelsea walikuwa wanaishi naye kama mkosaji haswa kocha Antonio Conte na kusisitiza kocha huyo hawezi kuwaweka wachezaji wake karibu.
Mahusiano mabovu kati ya Costa na Chelsea yalianza tangu mwezi wa kwanza lakini yakakolea zaidi baada ya ujumbe mfupi ambao inadaiwa Conte alimtumia Costa baada ya msimu wa ligi kuisha.
Nafasi ya Diego Costa katika kukosi cha Chelsea tayari ameshapewa Alvaro Morata lakini tangu ajiunge na klabu hiyo mambo yamekuwa magumu kiasi cha mashabiki wa timu hiyo kutamani Costa arudi.
Post a Comment