Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakivuna.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wameendelea na kuwekeza nguvu katika kilimo wakati huu ambao amestaafu majukumu yake ya Urais.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakivuna.
Rais Kikwete kutumia ukurasa wake wa instagram amepost picha nne akiwa shambani kwake Msoga Chalinze katika shamba la mahindi wakivuna, Kikwete alikuwa akivuna na mkewe Mama Salma Kikwete.
Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakibeba mahindi mwao.
 
Picha za mstaafu huyo ambaye ni kipenzi cha Watanzania zimekua gumzo mitandaoni na kusambaa kwenye magrupu ya WhatsApp huku kila mtu akifurahia kuona wastaafu wengi wakijituma na kuelekeza nguvu zao kwenye kilimo na wengine mifugo.