Header Ads

KIM NANA AFUNGUKA MKWANJA ANAOLIPWA


Video queen Bongo, Kim Nana.

LICHA ya mavideo queen wengi Bongo ku’feki mkwanja wanaolipwa kwa video huku wengine wakidai hulipwa hadi milioni tano, kwa upande wa video queen Bongo, Kim Nana amefunguka ukweli kuwa mara nyingi hupokea mkwanja kuanzia laki 3 kwa video.
                          Kim Nana akiwa katika pozi.
Akichonga na Over Ze Weekend, Kim Nana aliyeuza nyago kwenye video kibao Bongo zikiwemo za Beka Flavour wa Yamoto Band alisema, amekuwa akifanya kila kitu kwa uhalisia na siyo ku’feki kama wengine.
“Wengine wanaweza kudhani nilikimbia gemu noo! Nilikuwa nimebanwa na kampuni ambayo haikuwa ikitaka niendelee na kuuza nyago lakini sasa hivi mkataba nao nimeshamaliza na napiga video za watu kama kawa. Nikikamua nakamua kweli na gharama zangu siyo kama hao wengine wanaofeki, nachaji kuanzia laki 3 tu,” alisema Kim Nana.

No comments