Header Ads

MBAO FC WAPATA MKATABA WA SHILINGI MILIONI 140


Mbao FC baada ya kusaini mkataba na GF.
Mbao FC imesaini mkataba waudhamini wa mwaka mmoja na kampuni ya uagizaji wa magari ya mizigo GF Trucks & Equipmentswenye thamani ya shilingi milioni 140.
Akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ofisa masoko wa kampuni hiyo, Kulwa Bundala alisema ndani ya mkataba huo wataipatia klabu hiyo basi lenye thamani ya shilingi milioni 70 pamoja na fedha taslimu shilingi milioni 70.
Upande wa Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi ameishukuru Kampuni ya GF kwa kuingia nao mkataba huo na basi hilo litawasaidia katika safari mbalimbali kipindi hiki cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Huo unakuwa udhamini wa pili kwa washindi hao wa pili wa Azam Sports Federation Cup, baada ya mwaka jana kupata udhamini wa Hawaii Products Supplies, watengenezaji wa maziwa ya Cowbell wenye thamani ya shilingi milioni 50 kwa msimu.

No comments