Header Ads

Golikipa wa Simba anapelekwa India kutibiwa


Golikipa wa Simba na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Said Mohamed ‘Nduda’ anatarajiwa kwenda India kwa ajili ya matibabu ya goti.
Taarifa rasmi ya klabu iliyotolewa na afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara inaeleza kwamba, Nduda aliumia wakati wa maandalizi ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Nduda anatarajiwa kuondoka mwishoni wa juma hili kuelekea India kwa ajili ya matibabu zaidi ambapo inaelezwa kwamba atakaa nje ya uwanja kwa majuma manne hadi sita.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa, Haruna Niyonzima na John Bocco wameanza mazoezi na wachezaji wengine baada ya kupata majeraha madogo siku chache zilizopita.
Kwa upande wa Shomari Kapombe ambae anasumbuliwa na majeraha ya muda mrefu, anaendelea vizuri huku akitarajiwa kuanza mazoezi siku chache zijazo.

No comments