AMBER LULU AANIKA SABABU ZA KUSTAAFU KUUZA NYAGO
MWANADADA machachari Bongo, Lulu Eugen ‘Amber Lulu`ameamua kustaafu kazi ya u-video queen kutokana na watu wanavyoidharau kazi hiyo na kuamua kujikita kwenye muziki wa Bongo Fleva.
Akibonga na paparazi wetu juzikati, Amber anayetamba na wimbo wa Only You, alisema kwenye maisha mtu anapaswa kusonga mbele na siyo kurudi nyuma hivyo ameshavuka kwenye sekta ya kuuza nyago kwenye nyimbo za watu na kuamua kukomaa kwenye fani ya muziki.
“Sitarajii tena kuwa video queen kwenye nyimbo za watu, kwanza muziki unanilipa zaidi kuliko fani ya kuuza sura inayodharaulika, hata mtu anipe dau gani siwezi kuuza sura kwenye wimbo wake,” alisema Amber.
NA: MAYASA MARIWATA| AMANI
Post a Comment