Header Ads

NANDY AKESHA AKISALI ASIBUME


Nandy.
MSANII wa muziki Bongo, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kwa sasa anatumia muda mwingi kukesha kwenye maombi kwa lengo la kuendelea kung’arisha nyota yake, ikiwa ni pamoja na kutobuma kwa kazi zake.

Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Nandy ambaye kwa sasa anaserebuka sokoni kwa wimbo wa Wasikudanganye, alidai wasanii wengi wamekuwa wakirudi nyuma kimuziki na wengine kupotea
kabisa kutokana na kutodumu kwa kazi zao muda mrefu, hivyo kushindwa kufanya vizuri na mwisho wa siku kusahaulika kwa mashabiki.

Nandy akesha…

“Siku zote nasali, mashabiki zangu wanikubali kila nyimbo nitakayotoa, unajua kukubalika kwa kila wimbo unaotoa siyo kazi ndogo, nakesha nikimuomba Mungu na pia kujituma katika kazi,” alisema Nandy.

NA: MAYASA MARIWATA

No comments