Header Ads

Nina uhakika hujawahi kufahamu suala hili kuhusu Wayne Rooney na Everton


Bado siku 3 tu kwa ujio wa klabu ya Everton nchini Tanzania, sio mbali ni siku ya Alhamisi tu Everton watacheza katika uwanja wetu wa taifa katika maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya Uingereza.
Mashabiki wa soka Tanzania nzima wamekuwa na hamu kubwa kuishuhudia klabu hiyo huku gumzo kubwa likiwa ni uwezekano wa ujio wa Wayne Rooney aliyesajiliwa na klabu hiyo kutoka klabu ya Manchester United.
Rooney amerejea katika klabu yake hiyo ya zamani ambayo aliondoka mwaka 2004 na sasa baada ya miaka 13 anarejea Goodison Park ambapo inaonekana huenda ndio anaenda kumalizia maisha yake ya soka.
Wakati Wayne anasaini Everton ameongea kitu ambacho hakuna mshabiki wa soka ameshawahi kukijua, ni siri ambayo Wayne amekuwa nayo kipindi chote akiwa United na pengine ni mkewe na wanae tu ndio wanajua kuhusu hili.
Ni kwamba wakati Rooney alipokuwa akiichezea Manchester United, ukweli ni kwamba pamoja na kuvaa jezi ya Manchester United lakini usiku alikuwa akivaa nguo ya kulalia ya klabu ya Everton.
“Kiukweli nimekaa kimya kwa miaka 13 kuhusu hili lakini ukweli ni kwamba kila ikifika usiku nilikuwa navaa Pyjamas za klabu ya Everton, sio mimi tu bali hata wanangu walikuwa wakivaa Pyjamas za United” alisema Rooney.
Rooney amekubali kupunguza mshahara wake hadi £160,000 ikiwa ni pungufu ya karibia 50% ya alichokuwa akipewa United kwa wiki ili kurejea katika klabu hiyo ya Everton kwa dili lenye thamani ya £10m.

No comments