Header Ads

Chelsea waanza mazoezi, Costa aomba kutorudi


Klabu ya Chelsea leo imeanza mazoezi ya kujiandaa na msimu wake mpya wa ligi na wachezaji mbali mbali nyota akiwemo Willian na Pedro walionekana wakipasha na kikosi hicho.
Lakini wawakilishi wa mshambuliaji Diego Costa wametuma maombi kwa klabu ya Chelsea wakiomba mteja wao likizo yake iongezwe kidogo kwani kuna masuala yake binafsi anayashughulikia.
Inafahamika kwamba Diego Costa na Antonio Conte wana uhusiano mbovu kwa sasa na hiyo inaepelekea mshambuliaji huyo kuanza kufungasha virago vyake akitafuta pakwenda msimu ujao wa ligi.
Habari zaidi zinadai Costa anataka kurejea katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid na mazungumzo kati ya Atletico yanaendelea vizuri na ndio sababu ya mshambuliaji huyo kuomba muda wa ziada katika likizo yake.
Chelsea tayari wamejiandaa kuziba pengo la Costa kwani baada ya Lukaku kujiunga na Manchester United sasa klabu hiyo imehamisha majeshi kwa Alvaro Morata ambapo kiasi cha £70m kimetengwa kumnasa Mhispania huyo.

No comments