Header Ads

Hii ndiyo sababu ya Terry kusaini timu isiyocheza ligi kuu


John Terry alitangaza kuondoka katika klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita na leo ahadi ya Terry imetimia baada ya kusaini katika klabu ya Aston Villa.
Wengi wameshangazwa na kitendo cha Terry kukubali kwenda Aston Villa wakati klabu hiyo haishiriki ligi kuu na wanacheza katika ligi ya Championship.
Wengi waliamini kwa uwezo na uzoefu wa Terry huenda angejiunga na klabu nyingine ndogo zinazoshiriki ligi kuu ikiweml Watford ambao walitajwa kuhitaji saini yake.
Sababu kubwa Terry kusaini Aston Villa ni Chelsea, Terry anasema kucheza dhidi ya Chelsea ni kati ya vitu ambavyo amekuwa akiviwaza wakati akifikiria kuondoka.
“Akilini nilikuwa nawaza sana jinsi nitacheza dhidi ya Chelsea na hakika hiyo ingekuwa ngumu kwangu, kwa sasa niko hapa na nawatakia Chelsea kila la kheri katika msimu ujao” alisema Terry.
Kocha wa Villa Steve Bruce ndiye anatajwa kama mshawishi mkubwa kwa Terry kujiunga na Villa kwani tangu waonane nchini Ureno mwaka jana wawili hao wamekuwa wakizungumza sana na sasa wamekuwa pamoja.

No comments