Header Ads

SportPesa yaibeba Everton mbele ya United


                          Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza, Michael Keane

Klabu ya Everton ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha malipo ya pauni milioni 25 ya kumsaini beki wa timu ya taifa ya Uingereza, Michael Keane ambaye alikuwa akitakiwa na Man United.

 Keane mwenye umri wa miaka 24, anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya saa chache zijazo kabla ya kukamilisha uhamisho wake rasmi.
Everton inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa itatangaza rasmi usajili wa mshambuliaji kinda, Sandro Ramirez kutoka Malaga nichin Hispania.
Usajili wa wachezaji hao wawili utaifanya klabu hiyo kutumia zaidi ya pauni milioni 90, hata hivyo tayari imeshanasa saini ya mlindalango wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana walio na umri chini ya miaka 21, Jordan Pickford kwa kitita cha pauni milioni 30. Na kufanikiwa kumnunua nahodha wa klabu ya Ajax , Davy Klaaassen kwa uhamisho wa pauni milioni 24.
Kuwasili kwa Keane haitakuwa mwisho wa Everton kutumia pesa nyingi chini ya meneja Koeman, the Toffees pia watafanya biashara na burnley katika msimu wa majira ya joto baada ya ripoti kwamba wameanza mazungumzo dhidi ya mshambuliaji Andre Gray

No comments