Header Ads

Chicharito kurejea Epl?



West Ham wamefanya mazugumzo na klabu ya Bayer Leverkusen kuhusu usajili wa straika Javier Hernandez, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.
Straika huyo wa zamani wa Manchester United ana thamani ya pauni milioni 13 ambayo iliwekwa kwenye mkataba wake na kama West Ham kweli wanamtaka itawapasa kutoa kiasi hicho.
West Ham wana mpango wa kusajili angalau mshambuliaji mmoja majira haya ya kiangazi na Hernandez ni mshambuliaji mwenye uzoefu na ligi kuu ya Uingereza ambaye wanamuhitaji.
Hernandez amefunga mara 39 katika misimu miwili iliyopita katika klabu ya Leverkusen alihamia Ujerumani kutoka Man United mwaka 2015 kwa pauni milioni 7.3 na sasa yuko mbioni kurejea Uingereza.
West Ham pia wamefanya mazungumzo na Manchester City kuhusu Kelechi Iheanacho, Olivier Giroud wa Arsenal , straika wa Chelsea  Michy Batshuayi na Straika wa FC Cologne ya Ujerumani  Anthony Modeste.

No comments