Sipo tayari kusainiwa na label yoyote – Jay Moe
Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Jay Moe amefunguka kwa kudai kuwa hataki kusainiwa na label yoyote kwa kuwa ana mpango wa kuanzisha label yake itayokuwa inasaidia wasanii wachanga.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nisaidie Kushare’ amedai akiwa ndani ya label ya mtu mwingine atashindwa kufanya baadhi ya vitu ambavyo anafikiria kuvifanya.
“Mimi sipo kwa Mr T Touch wala sipo tayari kusainiwa na label label yoyote kwa sababu nina label ambayo anataka niikuze niwasaidie wengine ambao wapo nyuma yangu,” Jay Moe alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Moe amedai anaona kuna vijana wengi ambao wanahitaji msaada katika muziki hivyo mtu kama yeye akisainiwa sehemu kuna namna atashindwa kuwasaidia.
Post a Comment