Mayweather kutua Nigeria mwezi huu: Kuzichapa na spika wa bunge
Bondia mstaafu na bosi wa ‘The Money Team’ (TMT), Floyd Mayweather Jr anatarajia kutua nchini Nigeria Juni 12 hadi 14 mwaka huu na kuzichapa na Spika wa baraza la wawakilishi nchini humo, Yakubu Dogara kwenye pambano la hisani.
Floyd Mayweather Jr
Akizungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii mjini Lagos Mwenyekiti wa Tettrazzini Group of Companies, Kampuni mama ya Zzini Media ambao ni waandaaji wa ziara hiyo, Bw. Donatus Okonkwo amesema Mayweather atazichapa na Mh. Yakubu Dogara katika pambano la hisani lililoandaliwa na Baraza la wawakilishi (Bunge) nchini humo.
“Floyd anakuja kusini mwa jangwa la Sahara kwa mara ya kwanza na yeye na hii ni mara yake ya kwanza nchini Nigeria,tunawaomba wanigeria tujitokeze kwa kwa wingi”alisema Okonkwo.
Hata hivyo Floyd Mayweather amethibitisha taarifa hizo kwa kusema atakuwepo nchini humo june 12 hadi 14, huku mtandao wa Guardian ukiandika kuwa bondia huyo licha ya pambano hilo atatembelea mapango ya Ogbunike yaliyo kusini mwa nchi hiyo ambayo ni kivutio kikubwa cha watalii.
Post a Comment