Header Ads

Serikali yakiri upungufu wa nyumba za kuishi askari nchini


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amekiri tatizo la kuwepo kwa upungufu wa nyumba za askari nchini, huku akisema serikali kwa kufahamu hilo imekuwa ikitenga bajeti ya ujenzi wa makazi kwa awamu kulingana na uwezo uliopo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni
Hayo yamebainishwa na Mh. Masauni leo bungeni, Mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge Amina Mwakilagi lililohoji,
Je? Ni nini mipango ya serikali yakumaliza tatizo kubwa la nyumba za askari hapa nchini.
“Ni kweli kuna tatizo kubwa sana la nyumba za askari za kuishi, kwa kufahamu hilo Serikali imekuwa ikitenga bajeti ya ujenzi wa makazi kwa awamu kulingana na uwezo uliopo, aidha pamoja na kutenga fedha hizo wizara yangu itajielekeza zaidi kutumia rasilimali zilizopo na teknolojia rahisi za ujenzi wa nyumba ili kupunguza tatizo hili. kupitia ubia baina ya serikali na sekta binafsi, jeshi la polisi limefanikiwa kujenga nyumba 353 Kunduchi na Mikocheni Dar es salaam, kwaajili ya askari wa kawaida na maafisa,” alisema Masauni.
“Aidha jeshi la magereza linaendelea na ujenzi wa nyumba 320 Ukonga Dar es salaam, kwa fedha ya Serikali na pia lipo katika mazungumzo ya ubia na shirika la nyumba nyumba la taifa, utakao wezesha kujenga nyumba 100 Msalato Dodoma, kadhalika idara ya uhamiaji inafanya makubaliano na shirika la nyumba la taifa kwaajili ya ununuzi wa nyumba 301 Dodoma ikiwa ni utaratibu wa kuhamia Dodoma. Utaratibu huu utaendelezwa katika mikoa mingine ili kupunguza Changamoto hii ya askari wetu.”

No comments