Fahamu gari linalotumia injini ya ndege
Gari aina ya ‘Bloodhound’ linalotumia injini ya ndege aina ya Eurofighter-Typhoonl ndiyo gari lenye kasi zaidi duniani, kwa kudhihirisha hilo litafanya majaribiao yake ya kwanza ifikapo tarehe 26 Oktoba mwaka huu.
Bloodhound litafanya majiribio yake ndani ya uwanja wa ndege wa Newquay huko Conawall na litatumia kasi(speed) ya 763mph au 1,228km/h. Kwa sasa gari hilo litatumia kasi hiyo ila wahandisi wanafikiria kuliongezea kasi zaidi hadi 800mph na kisha 1000mph.
Ifikapo mwakani gari hilo linatarajiwa kufika eneo la Hakskeen Pan , Mashariki mwa Cape nchini Afrika Kusini, na litakaa huko kwa muda wa mwaka mmoja, Hata hivyo wahandisi wa gari hilo wanataka kukagua mitambo yote ya gari kabla ya kwenda Afrika Kusini.
Dereva aitwae Andy Green ndiye atakuwa dereva wa kwanza kulijaribu Bloodhound katika uwanja huo, Andy atalazimika kutumia kasi ya 200mph ilikuliendesha gari hilo, katika eneo la barabara ya mita 2,744 iliwezesha Bloodhound kushika kasi.
Post a Comment