Mzee Yusuf afiwa na mkewe
Mzee Yusuf akiwa na Mke wake Chiku enzi za uhai wake
Aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Taarabu nchini Tanzania, Alhaj Mzee Yusuf jana usiku amefiwa na mke wake wa pili wa ndoa ajulikanae kwa jina la Chiku Khamis baada ya upasuaji (Operation) uzazi kutokwenda salama.
Chiku Khamis ameacha watoto wawili wote wa kike na mazishi ya marehemu yanafanyika leo saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Bongo5 Media Group tunatoa pole kwa familia ya Mzee Yusuf, pia endelea kufuatilia kwa karibu mtandao wetu ili tuweze kukujuza yatakayojiri.
Post a Comment