Waziri Mkuu Aridhishwa Na Mradi Wa Ujenzi Wa ‘Termina lIII
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la
abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)
na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.
Mradi
wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika
Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 24 kwa wakati
mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka na kuwa na.
Waziri
Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema
amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kukuta
Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi.
“Serikali
imejiimarisha katika kuboresha usafiri wa anga, ambapo kukamilika kwa
jengo hili kutachangia ongezeko la ndege kubwa nyingi kutua nchini. Pia
sekta ya utalii nayo itaimarika kwa kuwa watalii wanaoingia nchini
wataongezeka.”
Amesema
mbali na ujenzi wa jengo hilo, pia Serikali inaendelea kuvikarabati
viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma, Iringa, Kilwa
Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na
Songea ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.
Akisoma
taarifa za ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi
Christianus Ako amesema mradi huo umeajiri wafanyakazi 1,400 kwa sasa na
wanatarajia kuongeza watumishi na kufikia 1,800.
Pia
wanatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa vya umeme
kuanzia Julai, 2018 kwa kuwa tayari utekelezaji wa kazi kubwa za ujenzi
wa mradi huo zimefanyika.
Post a Comment