Ujenzi wa reli ya kisasa Kutoa Ajira kwa Wananchi 600,000
Rais
John Magufuli amesema ujenzi wa reli ya kisasa nchini utatoa ajira za
moja kwa moja 30,000 na zisizo za moja kwa moja 600,000.
Akizungumza
leo Jumatano Machi 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo
kutoka Makutopora mkoani Dodoma hadi Morogoro, Rais Magufuli amesema
mbali na kutoa ajira, ujenzi huo ukikamilika utanyanyua uchumi wa nchi.
“Ujenzi
wa reli hii utasaidia kutunza barabara zetu kama mnavyojua nchi yetu
imepinga hatua katika ujenzi wa barabara. Barabara zetu hazidumu
kutokana na kubeba mizigo mizito ambayo inaweza kusafirishwa kwa njia ya
reli,” amesema.
“Uwapo
wa reli hii utapunguza gharama za ukarabati wa barabara zetu. Ujenzi wa
reli hii utatoa ajira za moja kwa moja 30,000 na zisizo za moja kwa
moja 600,000… juzi tuliambiwa sasa tumefikia watu milioni 55, watu
wanasema kwa nini tunazaliana, mimi nasema tuazaliane tu. Mnapokuwa
wengi mnakuwa na sauti. Katika jumuiya tulizopo sisi tupo wengi tuna
sauti, jambo la msingi tuchape kazi,” amesema.
Amewataka Watanzania kuacha kuogopa wingi wao na kwamba, jambo la muhimu ni kufanya kazi.
“Denmark
ina watu milioni tano lakini wakati mwingine inatoa msaada hata kwa
nchi kama Tanzania kwa sababu watu wake wanafanya kazi. Nchi nyingi
duniani zimeshindwa duniani kwa sababu zinakopa halafu zinapewa masharti
magumu. Sisi tumejenga kwa hela ndogo tofauti na ilivyotarajiwa,”
amesema.
Habari Na Ally Rashidi
Post a Comment