Rais Magufuli Awapa ONYO TRA
Rais
Dkt. John Magufuli amemuagiza Kamishna wa TRA, Waziri wa Fedha na
katibu mkuu kuenda kuishughulika Shirika la Mapato Tanzania (TRA) ili
iweze kuacha tabia zake chafu za kuwaongezea raia kodi za mapato pindi
wanapokwenda kupata huduma hizo.
Dkt.
Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kabla ya
kuweka jiwe la msingi wa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya 'Standard
Gauge' katika eneo la Ihumwa, Dodoma ambapo awamu ya kwanza
ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017, katika maeneo ya PUGU, Jijini Dar
es Salaam.
"Napenda
kuwahimiza watanzania wote kuendelea kulipa kodi ili kutekeleza miradi
ya maendeleo nchini pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.
"Pamekuwepo
na mtindo mtu anapokwenda kununua bidhaa anapewa risiti ya bei ndogo
badala ya risiti anayotakiwa kupewa. Mtoa risiti na mpokeaji wote kwa
pamoja wanaibia serikali na hivyo wanasababisha kuchelewesha maendeleo
ya kujenga reli, ninawaomba watanzania tuwe wazalendo", amesema Rais
Magufuli.
Pamoja
na hayo, Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "TRA muangalie kodi zenu
mnazozitoza, inawezekana nyingine ni kubwa mno kuliko miradi
wanayotekeleza wananchi badala ya kuwa motisha kwa walipa kodi inakuwa
kero kwao na badala yake wanabuni njia ya kukwepa kulipa kodi.
"Kwa
hiyo TRA mjipange vizuri maana Kuna watu TRA si watu wazuri, na saa
nyingine wanapokwenda kule wanaipaka matope serikali kwa kusema hii ndio
dhana ya hapa kazi tu kumbe wao wanafanyakazi ya kuiba taifa".
Kwa
upande mwingine, Dkt. Magufuli ameitaka TRA kuendelea kutoa elimu ya
mlipa mkodi kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa wanachi na waweze
kulipa kodi kwa heshima kwa taifa lake.
Habari Na Hamisi Bakari
Post a Comment