Tamko La Waziri Wa Afyaummy Mwalimu Kuelekea Maadhimisho Ya Siku Ya Kifua Kikuu Duniani Machi 24 – Leo Mjini Dodoma
# Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.
#
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa
zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na
Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.
#
Tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania
tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini
mwao.
# Kauli mbiu ya mwaka huu inasema *” Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB.”*
#Nchini Tanzania kila mwaka jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.
# Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele.
#
Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake
zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma
na Binafsi.
#
Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua
Kikuu nchini ikiwemo kuimarisha uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu
katika Vituo vya Afya.
#
Serikali na wadau mbalimbali tunaendelea na utekelezaji wa kampeni za
uhamasishaji na upimaji wa Wananchi katika maeneo ya migodi, makazi duni
kwenye miji mikubwa, magereza na shule za bweni.
#
Pia Serikali imezindua dawa mpya za TB za watoto ili kuhakikisha
zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani ( WHO), dawa hizo mpya ni
za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na tayari zimeshawasili
nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na Halmashauri zote
nchini.
#
Nawaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma
kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi
wa TB kikamilifu kabla ya kuanza masomo.
#Ni
marufuku kwa Madaktari kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima
wanafunzi husika. Kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa kwa
uzembe ambao hauwezi kuvumilika.
# Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.
#Mpaka
sasa takribani watoa huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii
ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili
kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika
maeneo yao.
Post a Comment