Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka leo Algeria kupitia Dubai, ambapo kinataraji kuwasili nchini Tanzania kesho mchana. Taifa
Stars ilikuwa Algeria kwa ajili ya mchezo wa kirafiki ambao ni wa
kalenda ya FIFA uliopigwa nchini humo kwenye Uwanja wa Julai 5. Katika
mchezo huo, Stars ilipoteza kwa jumla ya mabao 4-1 na kujiwekea
mazingira magumu ya kupanda katika viwango vya ubora wa soka Duniani. Stars
itakuwa ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo utakaopigwa Machi 27 2018 jijini Dar es Salaam.
Post a Comment