MAKAMU WA RAIS KUONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kamati ya Harambee hiyo, Hassan Msumari na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamis Mgoda. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog;0715264202,0689425467
Na Ally Rashidi
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa
Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.
Akizungumza
katika mkutano na wanahabari, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya
hiyo, Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema kuwa hafla hiyo itakayoanza leo
Ijumaa saa 12 jioni kwenye Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki, Dar es
Salaam itaambatana na chakula cha usiku kwa wageni waalikwa.
Hivi sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wanaohitaji
huduma za afya wamekuwa wakitumia hospitali teule ya Kanisa la Anglikana
ambayo imeingia mkataba na Serikali na kutokana na idadi ya wananchi wa
wilayani hapo hospitali hiyo imezidiwa.
Hayo
yamesemwa leo na Mhandisi Tumbo wakati akizungumzia harambee ya
kuchangisha fedha inayotarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.
Mhandisi
Tumbo amesema kutokana na Wilaya ya Muheza kutokuwa na Hospitali ya
Wilaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974, wananchi wamekuwa wakiteseka
pindi wanapohitaji huduma za afya na hivyo wakaamua kuchanishana fedha
ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.
Amefafanua
tayari wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Muheza mkoani Tanga na
Watanzania kwa ujumla wameanza kuchingiaa ujenzi huo na hadi kukamilika
kwake zinahitajika fedha Sh.bilioni 11.1, hivyo wakati wakisubiri fedha
za Serikali Kuu na zile za kwenye bajeti wameamua kuanza kwa kuchangisha
fedha hizo.
"Kesho
tutakuwa na harambee itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12
jioni ambapo wananchi wa Wilaya ya Muheza wanaoishi Dar es Salaam
pamoja na watanzania wengine tunaomba wajitokeze kuchanga fedha kwa
ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya.
"Mgeni
rasmi kwenye tukio hilo la harembee ya kuchangisha fedha atakuwa Makamu
wa Rais ,Mama Samia Suluhu Hassan. Kwa wachangiaji ambao tumewapa kadi
ya kuja kwenye harembee hiyo kila mchangiaji atachangia kuanzia
Sh.milioni moja kwa walio na kadi.Na wote ambao tumewaalika kesho wana
kadi za mualiko,"amsema.
Amefafanua
kwa wale ambao wanahitaji kadi ni vema wakawasiliana naye kwa kutumia
namba yake ya simu ya mkononi ya 0713 341937 ili wapatiwe kadi huku
akifafanua pia mbali ya wale ambao watafika kesho kwenye harambee hiyo
pia wameandaaa utaratibu mwingine wa kuchangia ujenzi huo.
Mhandisi
Tumbo amesema ili kufanikisha ujenzi huo wanapokea mchango wa kiasi
chochote cha fedha na hao wachangie kupitia Tigopesa au M-pesa kwa
kutumia namba 395533 ambayo kumbukumbu namba ya kampuni ni 123.
"Tunatambua
jitihada za Serikali katika kutatua changamoto kwenye sekta ya afya, na
hasa Muheza lakini kwa upande wetu tumeamua kuanza kwa kuchangishana,
wapo wanaotoa fedha, wapo wanaochangia kokote, mchanga , saruji na vifaa
vingine vya ujenzi.Tumeanza vizuri kwani tayari msingi wa wadi ya akina
mama na watoto umejengwa na lengo letu hadi Oktoba mwaka huu tuwe
tumekamilisha ili wananchi wapate huduma za afya.
"Tukifanikiwa
kuwa na Hospitali ya Wilaya Muheza mwananchi anayehitaji huduma za
matibabu ya afya atakuwa na nafasi ya kuchagua aende kwenye Hospitali ya
Anglikana au ya Wilaya.Niishukuru Hospitali ya Anglikana kutokana na
kutoa huduma za tiba kwa wananchi wa Muheza,"amesema Mhandisi Tumbo.
Pia
amesema wakati wanaendelea kutafuta fedha kujenga Hospitali ya Wilaya
ya Muheza, wanaendelea na jitihada za kujenga zahanati na ujenzi huo
unaendelea kwa kasi kutokana na wananchi kuhamasika kuchangia ili
kuondoa changamoto ya uhaba wa zahanati za vituo vya afya.
Baadhi ya waandishi wa habari walihudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya
Golden
Tulip katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Katikati ni Adam Ngamange
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita),
ambaye kwa asilimia kubwa alisaidia kuaandaa mkutano huo.
Sehemu ya wanahabari hao
Mkuu
wa Wilaya, Tumbo akifafanua jambo ambapo aliwaomba wananhi kujitokeza
kutoa michango kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo. Kulia ni Katibu
Tawala wa wilaya hiyo, Desderia Haule.
Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza akijibu maswali ya wanahabari
Wajumbe
wa Kamati ya Harambe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
kumalizika kwa mkutano na wanahabari kwenye Hoteli ya Golden Tulip,
katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Juma Mgazija,
Mwenyekiti wa Kamati, Hamis Mgoda, Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Mwanasha
Tumbo, Katibu Tawala wa Wilaya, Desderia Haule na Katibu wa Kamati,
Hassan Msumari.
Post a Comment