Header Ads

SportPesa wasitisha udhamini kwenye michezo nchini Kenya


                                                Ronald Karauri

Kampuni ya kubashiri michezo mbalimbali nchini Kenya ya SportPesa imesitisha udhamini wake kwenye michezo nchini humo kutokana na uamuzi wa Serikali kuongeza kodi hadi asilimia 35 kutoka asilimia 7.5 ya awali.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 02, 2017, Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa SportPesa, Ronald Karauri amesema wamelazimika kujiondoa kwa sababu hawawezi kudhamini michezo kama watatozwa asilimia 35.
Bw Karauri amesema jukumu hilo la kudhamini michezo wameiachia serikali kudhamini michezo hiyo ikiwemo Soka, Ndondi na Raga.
Miongoni mwa michezo itakayoathiriwa na uamuzi huo wa SportPesa ni mpira wa miguu, ndondi na mchezo wa raga (Rugby).
Kwa upande wa mpira wa miguu SportPesa walikuwa wanadhamini Ligi Kuu ya Kenya KPL, timu za Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars pamoja na ligi ya Super 8.

No comments