Header Ads

Rais Wa Simba Fc Alazwa Muhimbili.....Mahakama yaelezwa anasumbuliwa na Figo



MWENDESHA Mashtaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ,(Takukuru) , Leonard Swai ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa Hospital ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na Figo.

Aveva ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi ambapo anashtakiwa pamoja na Makamu rais wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alikuwepo mahakamani hapo

Wakili Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Amedai, walishachukua maelezo ya mshtakiwa wa pili na kwamba wanaangalia jinsi ya kupata maelezo ya mshtakiwa wa kwanza ambaye kwa sasa ni mgonjwa.Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa ameaihirisha kesi hiyo hadi February 8,2018 kwaajili ya kutajwa.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha Dola za kimarekani 300,000.

No comments