Header Ads

Rekodi inaibeba Yanga nyumbani vs Mbeya City


Leo Jumapili ya November 19, 2017 kikosi cha Yanga kitakuwa uwanja wa Uhuru kuikabili Mbeya City.  Yanga ina rekodi nzuri dhidi ya Mbeya City kwa mechi za Dar, imeshinda mechi tano zilizopita. Mbeya City haijawahi kushinda wala kutoka sare dhidi ya Yanga kwa mechi zilizochezwa Dar tangu klabu hiyo ilipopanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara mwaka 2013.
Yanga imeshinda mechi 4 zilizopita vs Mbeya City Dar
  • 2013/14 Yanga 1-0 Mbeya City
  • 2014/15 Yanga 3-1 Mbeya City
  • 2015/16 Yanga 3-0 Mbeya City
  • 2016/17 Yanga 2-1 Mbeya City
  • 2017/18 Yanga ?? Mbeya City
Yanga imeshinda mechi 1 kati ya 4 ilizocheza uwanja wa Uhuru
Kati ya mechi tisa ambazo Yanga imecheza hadi sasa, imecheza mechi nne kwenye uwanja wa Uhuru huku mechi tano ikicheza ugenini. Katika mechi nne ilizocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani (Uhuru) imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare katika mechi tatu. Si wastani mzuri sana kwa Yanga inapoutumia uwanja wake wa nyumbani.
  • Yanga 1-1 Lipuli
  • Yanga 1-0 Ndanda
  • Yanga 0-0 Mtibwa Sugar
  • Yanga 1-1 Simba
Yanga imeshinda mechi nyingi za ugenini kuliko nyumbani, imeshinda mechi tatu kati ya tano ilizocheza ugenini (Njombe Mji 0-1 Yanga, Kagera Sugar 1-2 Yanga, Stand United 0-4 Yanga) imetoka sare mbili katika mechi zake za ugenini (Majimaji 1-1 Yanga, Singida United 0-0 Yanga).
Yanga bila nyota watano kikosi cha kwanza vs Mbeya City
Yanga itacheza vs Mbeya City bila nyota wake watano ambao wanasumbuliwa na majeraha, Pappy Kabamba Tshishimbi, Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Amis Tambwe ni wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya timu ya Yanga itakayopambana dhidi ya Mbeya City.
Mbio za kuikamata Simba
Ushindi wa Simba jana dhidi ya Tanzania Prisons umeifanya Yanga na Mtibwa Sugar kuwa nyuma ya vinara hao wa VPL kwa pointi tano kabla ya michezo yao ya leo huku Azam wao wakiwa nyuma ya Simba kwa pointi tatu kabla ya mchezo wao wa leo ugenini dhidi ya Njombe Mji. Azam ndio timu pekee ambayo inaweza kuifikia Simba kwa pointi ikiwa itashinda mchezo wake wa leo, Yanga, Mtibwa, zitakuwa nyuma ya Simba kwa tofauti ya pointi mbili kama zikishinda mechi zao za leo.
Rekodi ya Mbeya City ugenini msimu huu
Haijashinda hata mechi moja kati ya nne ilizocheza ugenini msimu huu, imepoteza mechi mbili na kutoka sare michezo miwili. Inakutana na Yanga ambayo imeshinda mechi moja tu kati ya nne ilizocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani msimu huu.
  • Stand United 2-1 Mbeya City
  • Mwadui 2-2 Mbeya City
  • Mbao 2-2 Mbeya City
  • Azam 1-0 Mbeya City

No comments