Header Ads

Mourinho alivyoiboresha Man Utd baada ya Moyes na LVG – Jumapili darajani


Wakati akijibu maswali kuhusiana na kwamba kwanini Romelu Lukaku amekosa majukumu ya kupiga penati baada ya mchezo wa Jumanne iliyopita wa Champions League vs Benfica, Jose Mourinho alisema kitu ambacho kilionyesha umuhimu na nia yake ya kumaliza akiwa kinara katika kundi A.
Mara ya mwisho Manchester United walipokuwa kwenye Champions League, walimaliza nafasi ya 3, hivyo itakuwa jambo muhimu kumaliza na pointi 18 na tutajitahidi kufanikisha hilo.”
Alikuwa akitoa mfano wa msimu wa ulaya uliopita chini ya Louis van Gaal msimu wa 2015-16, wakati United waliposhinda mechi 2 katika mechi 6 za makundi na wakalosa nafasi ya kufuzu kucheza hatua ya 16 bora. Ulikuwa msimu ambao ulionyesha wazi msimu madhaifu ya timu baada ya kuondoka kwa Fergie: Performance mbovu katika mechi nyingi, matokeo mabovu.
Kulikuwa mpaka na vitu vya kuchekesha kama sio kuhuzunisha, huku Van Gaal akiwa sub ya kumuingiza Nick Powell katika hatua muhimu ya mechi ya mwisho dhidi ya Wolfsburg. Vitu vya namna hii ndio vilimfanya Mourinho awakumbushe walipotoka, United yake sasa ipo kwenye nafasi ya pili kwenye ligi na wapo mbioni kufuzi kucheza hatua ya 16 bora ya Champions League.
United wamefunga magoli 23 kwenye Premier League – idadi kubwa kuliko Tottenham, Chelsea, Liverpool na Arsenal na pia wameruhusu magoli machache kuliko timu nyingine yoyote kwenye ligi. Hawajaruhusu goli katika uwanja wa Old Trafford tangu mwezi April na ushindi vs Benfica ulikuwa mchezo wa 37 mfululizo bila kupoteza katika uwanja wa nyumbani, rekodi ambayo imedumu tangu September 2016. Ni mara moja tu kwenye enzi za Premier League – United wamekuwa na rekodi ya aina hii.
Ukiangalia vitu vyote lakini kuna baadhi ya mapungufu yanayoleta malalamiko kwa wakosoaji wa Mourinho, kama ilivyokuwa baada ya sare tasa dhidi ya Liverpool mnamo October 14, lakini yote ilitokana na imani kwamba Liverpool walikuwa dhaifu.
Gary Neville alikiambia kituo cha ESPN kwamba Sir Alex Ferguson kamwe asingelalamika na kuondoka na pointi 1 katika uwanja wa Anfield hasa mwanzoni mwa msimu. Sio siku nyingi sana Liverpool waliitandika United 3-0 katika uwanja wa Old Trafford na mashabiki wa ugenini walibeba bango lilosemeka “David Moyes is a football genius.”
Hivi sasa miaka 3 mbele, United wanaonekana kuwa miongoni mwa timu mbili zinazogombea ubingwa kwa nguvu, mara ya kwanza tangu Fergie alipostaafu. Tangu waliposhinda ubingwa wa 13 wa EPL mwaka 2013, wamemaliza nafasi ya 7, 4, 5, na 6 kwenye ligi ambayo sasa imekuwa na ushindani zaidi.
BIG 4 sasa sasa imekuwa Top 6. Ikimaanisha kwamba kuna mechi 10 za msimu za kucheza na timu zinazowania ubingwa; karibia 1/3 ya msimu imekuwa ngumu, michezo migumu kama ile ya Anfield. Mourinho ametengeneza sifa yake ya ukocha kwa kushinda mechi za namna hiyo na Jumapili hii tena atakuwa na mtihani mwingine darajani vs Chelsea.
Kwa mara nyingine tena, atafanya mambo kwa namna yake ambayo amekuwa akiitumikia kufanikisha mipango yake. Kama Gary Neville alivyozungumza kwenye kipindi cha Sky Sports cha Monday Night Football wiki hii: “Nadhani kwa sasa Manchester United wanahitaji mtu mwenye roho ngumu, mshindi anayepambana kwa kila hali. Ushindi wa mataji kwenye ligi 4 tofauti na mataji mawili ya Champions League- unaonyesha tayari wana mshindi wanamhitaji.
Timu za Mourinho zinashinda vikombe – hasa katika msimu wake wa pili — na kawaida hufikia kwenye hatua za mwishoni za Champions League. Kuna matagemeo ya namna hiyo kwa sasa, kwasababu ni Mourinho, kwasababu ni Manchester United.
Hata baada ya kupoteza vs Huddersfield- mwanzo huu wa msimu wa United ni moua ya mwanzo mzuri zaidi wa msimu tangu wakati wa Ferguson.
Baada ya kupata dhidi ya moja timu bora zaidi England wiki iliyopita huku akiwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu, wikiendi hii Mourinho anaelekea Stamford Bridge – uwanja ambao msimu uliopita alipoteza mechi mbili, moja ya kombe la FA, na nyingine ya ligi ambayo walipigwa 4-0. Kwa namna anavyofahamika Mourinho ataingia kwenye mchezo huu akiwa na mbinu ambazo zitakuwa tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita na huenda akapata matokeo chanya.
Japokuwa rekodi za United katika uwanja huo zinatia mashaka, tangu mwaka 2002 – takribani miaka 15 iliyopita- Red Devils wameshinda mechi moja tu ya ligi – wamecheza jumla ya mechi 15, wameshinda 1, sare 5 na wamefungwa 9.

No comments