Header Ads

Licha ya kusumbuliwa na warembo bado Lava Lava yupo single


Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Lava Lava amesema licha ya kusumbuliwa na warembo kwa sasa yupo single.
Muimbaji huyo amesema kutokuwa katika mahusiano kuna sababishwa na kushindwa kuelewa yupi mkweli kwani wengi wanafuata umaarufu alionao kwa sasa.
“Sana sana, unajua kwa sababu gani?, kabla sijatoa tuachane nilikuwa nimeachana na mpenzi wangu baada ya kutoa wimbo kuna wanawake wengi wanakuja lakini wote wanaokuja ni kwa sababu wewe ni Lava Lava” Lava Lava ameiambia Radio Free Africa.
Hadi sasa chini ya usimamizi wa label ya WCB Lava Lava ameweza kutoa ngoma mbili ambazo ni Dede na Tuachane ambayo ndio official.

No comments